Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema mchezo wa ‘Deby’ hautabiliki na lolote linawezekana lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda kesho.
Robertinho amesema Simba ni timu kubwa na inahitaji kushinda kila taji lililo mbele yake na ndicho tunapaswa kukifanya kesho.
Akizungumzia mchezo wenyewe Robertinho amesema utakuwa mgumu na tunategemea kupata upinzani lakini tutaingia uwanjani kwa jambo moja kwenda kutafuta ushindi.
“Derby ni Derby na siku zote haitabiliki, tunafahamu itakuwa mechi ngumu na tunaiheshimu Yanga lakini tupo tayari kuhakikisha tunashinda.
“Pamoja na ugumu utakaokuwepo lakini tumejiandaa kuhakikisha tunashinda na kuchukua taji,” amesema Robertinho.
Kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, Israel Patrick amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika kilichobaki ni kwenda kutimiza majukumu yao kesho.
“Kwa upande wetu wachezaji tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, tunafahamu itakuwa mechi ngumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunawapa furaha mashabiki wetu,” amesema Israel.