Robertinho afurahishwa na ushindi

 

Kocha Mkuu Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema ushindi wa mabao 3-2 tuliopata leo dhidi ya Mbeya City ni jambo la kwanza alilokuwa anahitaji na limemfanya afurahi.

Robertinho amesema amefurahishwa na wachezaji walivyocheza kitimu licha ya kuwa amekaa nao kwa muda mfupi.

“Ilihitajika ushindi bila kujali tumechezaje, tupo kwenye mbio za ubingwa tunapaswa kushinda kila mchezo hasa tukiwa nyumbani.

“Ndiyo kwanza nina siku nane tangu nilipoanza kazi. Simba ni timu kubwa na malengo yake ni makubwa pia kama nilivyo mimi.

“Jambo jengine lililonifurahisha ni jinsi tulivyocheza, wachezaji walicheza kitimu ingawa kulikuwa na makosa kadhaa ambayo tunapaswa kuyaondoa.

“Nimeanza kupata mwanga wa kikosi ambavyo kinapaswa kiwe,” amesema Robertinho.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER