Robertinho afurahishwa na timu licha ya kupoteza dhidi ya Turan

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema amefurahi kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wetu licha ya kupoteza kwa bao moja dhidi ya Turan PFK katika mchezo wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Soğuksu Spor Kompleksi.

Robertinho amesema tulicheza vizuri kuanzia kwenye kushambulia, kuzuia pamoja na kumiliki mchezo kwa muda mrefu.

Robertinho ameongeza kuwa ubora wa kikosi tulionao sasa anaamini tutafanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika pamoja na mashindano ya ndani msimu ujao.

“Kwangu siangalii matokeo ya mwisho bali mchezo wenyewe ulivyokuwa. Tumecheza vizuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.

“Wachezaji wameonekana wapo timamu kimwili, kimbinu na hilo ni jambo ambalo limenifurahisha. Nawapongeza pia wasaidizi wangu wamefanya kazi kubwa kwa muda mfupi,” amesema Robertinho.

Robertinho ameweka wazi kuwa tunahitaji kucheza mechi nyingine moja ya kirafiki mwishoni mwa juma kabla ya timu kurejea jijini Dar es Salaam.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER