Robertinho afurahia Hali ya Kikosi

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefurahishwa na kiwango kilichoonyeshwa na wachezaji wetu katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Power Dynamos kwenye kilele cha Simba Day.

Robertinho amesema kikosi kinazidi kuimarika siku hadi siku na wachezaji wanazidi kuzoeana kitu ambacho kinampa wigo mpana wa uchaguzi wa timu.

Robertinho ameongeza kuwa wachezaji wapya waliosajiliwa wameonyesha uwezo mkubwa na wanazidi kuzoea mazingira ya timu pamoja na wenzao.

“Nimefurahishwa na kiwango cha timu, tumecheza vizuri na timu inazidi kuimarika. Tuna kikosi kizuri.

“Hata wachezaji wapya tuliowasajili wameonyesha uwezo mkubwa, na wanazidi kuzoea mazingira mapya pamoja na wenzao,” amesema Robertinho.

Robertinho amewashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la Simba Day na kulifanya kupendeza zaidi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER