Robertinho afafanua sababu ya kutoanza na namba tisa dhidi ya Al Ahly

Kocha Mkuu, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amefafanua kuwa sababu ya kutoanza namba tisa asilia katika mchezo wa ufunguzi wa African Football League (AFL) dhidi ya Al Ahly ni kutokana na ubora wa miamba hiyo kutoka Misri.

Katika mchezo huo ulimalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 Robertinho aliwaanzisha viungo washambuliaji Kibu Denis, Luis Miquissone, Clatous Chama na Saido Ntibazonkiza huku akiwaacha washambuliaji wote benchi.

Robertinho amesema Al Ahly ni timu bora na yenye uzoefu na michezo mikubwa wanapiga piga fupi fupi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza hivyo tulipaswa kuwa wengi katikati ili kupunguza mianya.

Robertinho ameongeza kuwa kila mchezo una mipango yake kwahiyo leo tulipanga kucheza hivi na wachezaji wangu wamejitahidi kuonyesha uwezo.

“Simba ina imesajili wachezaji 28, hao wote huwezi kuwatumia pamoja kwenye mechi moja. Wachezaji wanapangwa kutokana na aina ya mechi.

“Leo hatukuwa na namba tisa lakini Jean Baleke, John Bocco na Moses Phiri walikuwa benchi kutokana na aina mechi iliwahitaji zaidi viungo kuliko washambuliaji,” amesema Robertinho.

Akizungumzia mchezo wenyewe ulivyokuwa Robertinho amesema “tulicheza vizuri zaidi kipindi cha pili, tulifanya kila kitu sahihi na wenzetu Al Ahly walikuwa bora cha kwanza.”

Kuhusu mchezo wa marudiano kule Misri Robertinho amesema “siku zote mimi ni mtu chanya, siwezi kuzungumzia mchezo ambao hatukucheza lakini malengo yetu ni kushinda ugenini.”

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER