Mgeni Rasmi wa Mkutano wetu mkuu ambao utaanza muda mfupi ujao Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mh. Amos Makala amewasili Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC).
Mh. Makala amepokelewa na Mtendaji Mkuu wa Klabu, Imani Kajula na kumuongoza sehemu ambayo anatakiwa kukaa.
Pamoja na mambo mengine, zoezi la uhakiki wa wanachama ambalo lilianza tangu saa moja asubuhi bado linaendelea.