Rasmi tumetinga hatua ya makundi Mabingwa Afrika

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika baada ya kuifunga Premiero De Agosto kutoka Angola bao moja katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Tumeingia katika hatua hiyo kwa jumla ya mabao 4-1 kufuatia ushindi wa 3-1 tuliopata katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Novemba 11 nchini Angola wiki iliyopita.

Mchezo ulianza kwa kasi tukiliandama lango la De Agosto tukitafuta bao la mapema tukitengeneza nafasi kadhaa za kufunga lakini hakutuzitumia vizuri.

Mshambuliaji kinara Moses Phiri alitupatia bao la kwanza dakika ya 33 baada ya kupokea pasi ya Mohamed Hussein na kupiga shuti kali la chini chini lililomshinda mlinda mlango wa De Agosto.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo dakika 10 za mwanzo De Agosto walitushambulia mara kadhaa lakini safu yetu ikiwa imara nasi tukijibu mapigo lakini hata hivyo matokeo hayajabadilika.

Kocha Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwaingiza Kibu Denis, Habib Kyombo, Gadiel Michael, Jonas Mkude na Erasto Nyoni na kuwatoa Pape Sakho, Augustine Okrah, Mohamed Hussein, Israel Patrick na Henock Inonga.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER