Rasmi Simba ndani ya Makumbusho ya Taifa

Tumekuwa klabu ya kwanza Tanzania kuweka taarifa na kumbukumbu zetu kwenye Makumbusho ya Taifa ili vizazi vya sasa na vijavyo kupata nafasi ya kutembelea na kufahamu tulipotoka, tulipo na tunapoelekea.

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi, CPA, Issa Masoud amezindua eneo maalum ndani ya Makumbusho ya Taifa ambapo kumbukumbu zote za klabu yetu zimewekwa rasmi.

Baada ya kuzindua eneo hilo ambalo kuna eneo maalum taarifa zote za klabu tangu ilivyoanzishwa mwaka 1936, CPA Masoud
ametembezwa maeneo mbalimbali na Mkurugenzi wa Wanachama, Mzee Khamis Kisiwa.,

CPA, Masoud amesema tumeamua kuiweka historia ya klabu yetu ili kutunzwa ndani ya Makumbusho ya Taifa ambapo tunaamini itakuwa salama.

“Kuanzia sasa historia ya Simba inapatikana ndani ya Makumbusho ya Taifa, yoyote ambaye anataka kuijua vizuri Simba anapaswa kuja hapa na kujifunza,” amesema CPA, Masoud.

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Dk. Gwakisa Kamatula amewakaribisha Wanasimba na Watanzania kwa ujumla kutembelea ili kujua historia ya Simba tangu ilivyoanzishwa na mabadiliko mbalimbali iliyopitia hadi kufika sasa.

“Tunawaalika Wanasimba na Watanzania wote kuja kuifahamu timu hii kubwa Afrika. Kama kuna mtu ana picha au kipande cha gazeti, jezi ya miaka ya nyuma au viatu avilete hapa ili tuvihifadhi kwa kumbukumbu za sasa na baadae,” amesema Dk. Gwakisa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER