Rasmi Peter Banda asaini Simba

Kiungo Peter Banda raia wa Malawi amejiunga na kikosi chetu kutoka Timu ya Big Bullet, kwa mkataba wa miaka mitatu.

Banda ambaye anaweza kucheza nafasi nyingi za ushambuliaji anakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa nasi msimu huu.

Msimu uliopita Banda alikuwa akicheza timu ya FC Sheriff Tiraspol ya Moldova kwa mkopo akitokea Big Bullet.

Kuelekea msimu mpya wa ligi 2021/22, tumepanga kufanya usajili wa kisayansi ili kuboresha kikosi huku dhamira ya kwanza ikiwa ni kutetea ubingwa pamoja na kufanya vizuri kwenye michuano ya Klabu Bingwa Afrika.

Leave a comment