Rasmi Onana ni Mnyama

Uongozi wa klabu umefikia makubaliano ya kumsajili kiungo mshambuliaji Willy Essomba Onana (23) raia wa Cameroon kwa mkataba wa miaka miwili.

Onana amesajiliwa kutoka Rayon Sports ya Rwanda ambapo msimu uliopita ameibuka mchezaji bora wa ligi kuu nchini humo (MVP).

Onana ni mchezaji mwenye kipaji na uwezo mkubwa wa kucheza nafasi za mbalimbali uwanjani winga zote mbili pia anaweza kumudu nyuma ya mshambuliaji (namba 10) pia mshambuliaji kivuli (False number nine).

Msimu uliopita Onana aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu nchini Rwanda baada ya kufunga mabao 16 na kusaidia kupatikana kwa mengine matano (Assist)

Onana ndiye ingizo jipya la kwanza kikosini kwetu ikiwa ni sehemu ya maboresho kuelekea Msimu Mpya wa Ligi 2023/24.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER