Rasmi Mo aweka Bilioni 20 za uwekezaji Simba

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Mohamed Dewji ‘Mo’ leo ameweka shilingi bilioni 20 kwa ajili ya uwekezaji baada ya mchakato wa mabadiliko uliodumu kwa miaka minne kukamilika rasmi.

Baada ya Tume ya Taifa ya Ushindani (FCC) kuruhusu mchakato uendelee kufuatia kila kitu kukamilika Mo ameweka kiasi hicho cha pesa kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba yaliyowekwa miaka minne iliyopita.

Mo ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu Hassan na wote walioshiriki kufanikisha jambo hili kukamilika na Simba inaenda kuwa kubwa zaidi Afrika.

Mo ameweka wazi kuwa malengo yetu ya baadae ni kuhakikisha tunakuwa na Viwanja nane, kikubwa kwa ajili ya timu, cha timu ya vijana na wanawake ili kushindana kiukweli na klabu kubwa za Afrika kama Al Ahly, TP Mazembe, Waydad.

“Nilikuwa nakasirika sana nikisikia watu wakisema eti sina bilioni 20 za kuwekeza Simba. Kwa miaka minne wakati wa mchakato huu nimetumia bilioni 21.3 kwa kusajili, kulipa kambi, Pre Season, maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga n.k lakini hizo hazipo kwenye mkataba.

“Lakini baada ya kila kitu kukamilika leo nimetoa cheki ya bilioni 20 kwa Simba na zile zilizotumika hazihesabiki,” amesema Mo Dewji.

Kuhusu usajili Mo ameweka wazi kuwa utakuwa mkubwa msimu ujao na malengo yetu sio kuishia robo fainali tena Afrika badala yake tunahitaji kuchukua ubingwa wenyewe.

SHARE :
Facebook
Twitter

2 Responses

  1. NAIPENDA SANA SIMBA SPORTS CLUB
    Ninatamani siku moja nichangie kwa namna moja ama nyingine kuikuza SIMBA yetu iendelee kusonga mbele, timu ya bara la Africa.
    Daima msimbazi ni mafanikio kwanza! Nguvu moja.
    Nakupenda SIMBA SPORTS CLUB 🦁💖

    Regards,
    Moses Mataba
    Sales Executive @KAMAKA Co Ltd

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER