Klabu yetu imefikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Habibu Kyombo, kutoka Mbeya Kwanza kwa mkataba wa miaka miwili.
Kyombo anakuja kuboresha na kurudisha makali ya safu yetu ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya wa ligi 2022/23.
Katika msimu uliopita akiwa na Mbeya Kwanza, Kyombo amefunga mabao sita na kusaidia kupatikana kwa bao moja.
Kyombo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa ndani ya kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa ligi baada ya Mzambia, Moses Phiri kutoka Zanaco FC.
Kyombo anauzoefu mkubwa na soka la Tanzania, akiwa amechezea vilabu kadhaa kwa vipindi tofauti kabla ya kwenda Afrika Kusini.