Rasmi Chilunda ni Mnyama

Mshambuliaji, Shaban Idd Chilunda amejiunga nasi kwa mkataba wa miaka miwili akiwa mchezaji huru.

Chilunda ni miongoni mwa washambuliaji wazawa wenye vipaji na uwezo mkubwa na tunaamini atakuwa msaada kwenye kikosi.

Kwa nyakati tofauti Chilunda ameichezea Azam FC tangu akiwa kijana mdogo.

Chilunda ni miongoni mwa wachezaji wazawa waliofanikiwa kucheza soka la kulipwa ambapo amewahi kuzitumikia, CD Tenerife na CD Izarra zote za Hispania pamoja na Moghreb Tetouan ya Morocco.

Baada ya kusajiliwa Chilunda amewaomba Wanasimba tumpokee kwa mikono miwili pamoja na kumuombea ili atimize malengo ya klabu pamoja na yake.

“Sina mengi ya kusema bali Wanasimba wanipokee na waniombee, nimekuja kufanya kazi Simba nitajihid kwa kushirikiana na wachezaji wenzangu kuweza kushinda kila mechi na mataji klabuni,” amesema Chilunda.

 

 

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER