Rasmi Abdulsamad ni Mwekundu

Kiungo mkabaji Abdulsamad Kassim Ally, amejiunga na kikosi chetu akitokea Kagera Sugar tayari kwa ajili ya msimu mpya wa ligi 2021/22.

Abdulsamad amelivutia benchi la ufundi chini ya Kocha Didier Gomes kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha akiwa Kagera.

Tayari Abdulsamad yupo nchini Morocco pamoja na kikosi kilichoweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi.

Abdulsamad amekuja kucheza nafasi ya kiungo wa ulinzi pamoja na nyota kama Taddeo Lwanga, Jonas Mkude na Mzamiru Yassin

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER