Rais Samia Mgeni rasmi Simba Day

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan atakuwa mgeni rasmi katika kilele cha Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumapili, Agosti 6 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Simba Day ya mwaka huu ni kubwa na
maalum ndio maana tumemuomba Rais Dk. Samia kuwa mgeni rasmi.

Uongozi wa klabu unamshukuru Rais Dk. Samia kukubali mwaliko wetu nakuwa miongoni mwa Watanzania 60,000 watakao hudhuria Simba Day ya mwaka 2023.

Maandalizi ya Tamasha hili la kihistoria yanaendelea vizuri, kila kitu kipo kwenye mstari huku taratibu zikiwa vizuri ikisubiriwa siku yenyewe kufika.

Tayari tiketi za Tamasha zimeuzwa zote hivyo ni wazi mashabiki 60,000 wamethibitishwa kuhudhuria Simba Day 2023 ikiwa ni historia mpya kwakuwa haijawahi kutokea.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER