Rais Samia atuma salamu za pongezi za Simba Day

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pongezi kwa Wanasimba wote kwa kufanikisha Tamasha bora la Simba Day mwaka 2024.

Rais Samia ameongea na Wanasimba moja kwa moja baada ya kumpigia simu Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa akiwa ndani ya Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Rais Samia ametupongeza kwa kuendelea kulifanya Tamasha la Simba Day kuwa bora kila mwaka.

“Hongereni sana Wanasimba kwa Tamasha bora la Simba Day. Mwaka jana tulikuwa wote lakini leo imeshindikana kutokana na ratiba kuwa ngumu nimeshindwa kuwa hapo.”

“Nafahamu msimu uliopita hamkuwa bora sana lakini yaliyopita si ndwele, nyanyukeni songeni mbele,” amesema Dkt. Samia

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER