Quuens yapangwa Kundi A Mabingwa Afrika

Timu yetu ya Simba Queens imepangwa kundi A katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo itafanyika nchini Morocco Oktoba 31 hadi Novemba 13.

Queens ambayo inawakilisha Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) imepangwa na timu za Afsa FC (Morocco), Green Buffalo (Zambia) na Determine Girls (Libya).

Hii ni mara ya kwanza ya kikosi cha Queens kushiriki michuano hiyo mikubwa Afrika kwa Wanawake ambapo pia kwa Tanzania ni timu ya kwanza kufanya hivyo.

Queens ilipata nafasi hiyo baada ya kuifunga SHE Corporates kutoka Uganda katika mchezo wa Fainali ya Michuano ya CECAFA iliyofanyika Uwanja wa Azam Complex mwezi uliopita.

Michuano hiyo itashirikisha timu nane kutoka barani Afrika ambazo kila moja inawakilisha ukanda wake.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER