Queens yawaita mashabiki Uhuru kusherehekea ubingwa

Meneja wa timu ya Simba Queens, Seleman Makanya amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho dhidi ya Baobab Queens utakaopigwa Uwanja wa Uhuru kwa kuwa utatumika kukabidhiwa ubingwa wetu.

Makanya amesema itakuwa vizuri kama mashabiki watakuja kwa wingi wakati tunakabidhiwa taji la ubingwa kwa ajili ya kusherehekea jitihada tulizofanya kwa msimu wa 2021/22.

Makanya ameongeza baada ya kukamilika kwa msimu kesho wachezaji watapewa mapumziko ya siku chache kabla ya kuanza maandalizi ya michuano ya CECAFA.

“Kesho tutashuka dimbani kucheza na Baobab katika uwanja wa Uhuru, mchezo huu utatumika pia kukabidhiwa ubingwa na kufunga msimu wa ligi.

“Itapendeza kama mashabiki wetu watakuja kwa wingi kuwalaki wachezaji ambao wamefanya kazi kubwa mpaka kutwaa ubingwa. Nawasisitiza tu mashabiki waje kwangu,” amesema Makanya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER