Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens, imekamilisha usajili wa mshambuliaji Ibinabo Alex kutoka Confluence Queens FC ya Nigeria.
Mshambuliaji huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuhudumu kwenye kikosi chetu tayari kwa msimu mpya wa ligi 2022/23.
Confluence inashiriki Ligi Kuu ya Wanawake nchini Nigeria ambapo Ibinabo alikuwa mchezaji bora wa kikosi.
Queens inajipanga kwa ajili ya michuano ya CECAFA ambayo itaanza kutimua vumbi siku chache zijazo.