Queens yavunja kambi

Timu yetu ya Simba Queens leo imevunja kambi baada Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier) kusimama kupisha mechi za kimataifa.

Wachezaji wamepewa mapumziko ya wiki ya mbili huku wale walioitwa timu zao za taifa wakiruhusiwa kwenda kujiunga nazo.

Meneja wa timu Selemani Makanya amesema baada ya mapumziko hayo wachezaji watarejea mazoezini tayari kwa maandalizi ya ligi mzunguko wa pili.

“Leo tumevunja kambi yetu, wachezaji wamepewa mapumziko ya wiki mbili na wale walioitwa timu zao za taifa wamepewa ruhusa ya kwenda kujiunga nazo,” amesema Makanya.

Katika Ligi hiyo ya Wanawake tumemaliza mzunguko wa kwanza tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha pointi 33 na kushinda mechi zote 11

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER