Queens yatwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii

Timu yetu ya Simba Queens imetwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii baada ya kuifunga JKT kwa mikwaju ya penati 5-4 katika mchezo wa fainali uliopigwa Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ulienda kwenye hatua ya penati baada ya kumalizika kwa sare ya bao moja katika dakika 90 za kawaida.

Stumai Abdallah aliwapatia JKT Queens bao la kwanza kwa kichwa dakika ya 20 akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Jonesia Minja.

Danai Bhobo alitupatia bao la kusawazisha dakika ya 27 baada ya mpira wa kona uliopigwa na Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ kuokolewa na mlinda mlango wao JKT kabla ya kumkuta mfungaji.

Kocha Mkuu, Juma Mgunda alifanya mabadiliko ya kuwatoa Dotto Evarist, Mwanahamis Omary, Ritticia Nabossa, Elizabeth Wambui na kuwaingiza Aisha Juma, Joelle Bukuru, Olaiya Barakat, Daniela Ngoyi.

Penati zetu zote tano zilifungwa na

Daniella Ngoyi, Aisha Juma, Joelle Bukuru
Ruth Ingosi, Vivian Corazone huku zile za JKT zikifungwa na Esther Mabanza, Anastazia Katunzi, Crista John, Jonesia Minja.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER