Queens yatinga Nusu Fainali Mabingwa Afrika kibabe

Kikosi chetu kimefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuifunga Green Buffaloes kutoka Zambia katika mchezo wa mwisho wa Kundi A.

Katika mchezo huo, Djafar alipoteza nafasi ya wazi dakika ya 43 baada ya shuti lake la chini chini kutoka nje kidogo ya lango akiwa anatazamana na mlinda mlango baada ya kupokea pasi ya Opa Clement.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kuliandama lango la Buffalos ambapo dakika ya 64 Djafar alitupatia bao la kwanza kwa kichwa akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Fatuma Issa ‘Fetty Densa’.

Nahodha Opa Clement alitupatia bao la pili dakika ya 79 baada ya kupokea pasi ndefu ya mpira wa kutengwa iliyopigwa na mlinzi wa kati Daniela Kanyanya.

Agnes Musase wa Green Buffaloes alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu dakika ya mwisho ya baada ya kumfanyia madhambi Opa.

Ushindi huu unatufanya kumaliza kundi kwa kufika alama sita tukiwa nafasi ya pili nyuma na wenyeji ASFAR FC ambao ndiyo vinara wakiwa na alama tisa.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Philomena Abakah, Olaiya Barakat, Pambani Kuzoya na Diana Mnali na kuwaingiza Asha Djafar, Amina Hemed, Vivian Corazone na Dotto Evarist.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER