Queens yatinga Nusu Fainali CECAFA

 

Ushindi wa mabao 2-0 uliopata Tinu yetu ya Wanawake ya Simba Queens dhidi ya SHE Corporates ya Uganda imetufanya kutinga Nusu Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwenye Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex ulikuwa mgumu timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini tulikuwa bora zaidi ya mabingwa hao wa Uganda.

Vivian Corazone alitupatia bao la kwanza dakika ya 21 akimalizia mpira wa adhabu uliopigwa na na kiungo Joelle Bukuru.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo Pambani Kuzoya alitupatia bao la pili dakika ya 61 na kutuhakikishia ushindi.

Katika mchezo wa kwanza tulipata mshindi mnono wa mabao 6-0 dhidi ya Garde Publicaine ya Djibouti hivyo ushindi wa leo unatufanya kutinga hatua inayofuata.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Philomena Abakah, Asha Djafar, Diana William na Vivian Corazone na kuwaingiza Olaiya Barakat, Aisha Juma, Silvia Mwacha na Sarrive Badiambila.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER