Queens yatimiza ahadi ya kushinda mechi zote mzunguko wa kwanza

Ushindi wa mabao 3-1 tuliopata dhidi ya Fountain Gate katika Uwanja wa Mo Simba Arena umetufanya kutimiza ahadi ya kushinda mechi zote za mzunguko wa kwanza wa Serengeti Lite Women’s Premier League.

Jana, Kocha MkuuSebastian Nkoma alisema malengo yetu ni kuhakikisha tunashinda mechi zote za mzunguko wa kwanza na leo tumefanikiwa.

Mchezo wa leo ulianza kwa kasi huku tukiliandama lango la Fountain Gate ambapo dakika ya 15 tulifanikiwa kupata bao lililofungwa na Olaiya Barakat.

Baada ya bao hilo tuliendelea kushambuliana kwa zamu lakini Fountain walifanikiwa kusawazisha dakika ya 37.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo dakika ya 69 Amina Ramadhani alitupatia bao la pili baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Fountain.

Opa Clement alitupatia bao la tatu dakika ya 88 baada kumalizia mpira wa krosi iliyopigwa Mercy Tagoe.

Ushindi huu umetufanya kumaliza mzunguko wa kwanza wa ligi kwa kudhinda mechi zote 11 na kujikusanyia alama 33 na kuendelea kukalia usukani.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER