Queens yatamba kuchukua ubingwa mara tatu mfululizo

Kocha Mkuu wa Timu ya Wanawake ya Simba Queens, Sebastian Nkoma ameweka wazi kuwa malengo yetu ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) kwa mara ya tatu mfululizo.

Nkoma ametoa kauli hiyo mbele ya waandishi wa habari wakati akielezea maandalizi ya mchezo wetu wa Derby dhidi ya Yanga Princess utakaopigwa Jumapili Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Nkoma amesema tutaingia katika mchezo huo bila kuangalia historia kwa kuwa tumewafunga Yanga mechi zote tulizokutana ila tutachukua tahadhari sababu tunahitaji kupata alama tatu.

“Lengo letu ni kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho sababu tunahitaji kushinda taji la Ligi Kuu kwa mara ya tatu mfululizo. Mchezo utakuwa mgumu hii Derby lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda,” amesema Nkoma.

Kwa upande wake Nahodha, Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ amesema wachezaji hawana presha licha ya kuwa ni mchezo mkubwa na tumejiandaa vizuri kupata alama tatu.

“Ikishaitwa Derby ni mechi ngumu, tunategemea kupata upinzani mkubwa kutoka Yanga lakini tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunashinda,” amesema Fetty Densa.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER