Kikosi chetu cha Simba Queens kimekamilisha usajili wa mshambuliaji Philomena Abakah kutoka Berry Ladies inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ghana.
Usajili wa Philomena unakuwa wa tatu kuelekea msimu mpya baada ya Ibinabo tuliye mtambulisha jana na Zainabu Mohamed.
Jana tulikamilisha usajili wa mshambuliaji Ibinabo Alex kutoka Confluence Queens FC ya Nigeria.
Tunaendelea kuimarisha kikosi chetu kuelekea msimu ujao wa ligi pamoja na michuano ya CECAFA ambayo itaanza mwishoni mwa mwezi huu jijini Arusha.
Malengo yetu ni kuhakikisha tunakuwa na timu imara ambayo utatuwezesha kutetea ubingwa wetu wa Serengeti Lite Womens Premier League.