Timu yetu ya Simba Queens imekamilisha usajili wa mshambuliaji Ainembabazi Joanitah raia wa Uganda kwa mkataba wa miaka miwili.
Ainembabazi anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa msimu huu kutoka Uganda baada ya jana kumtangaza Nabbosa Ritticia ambaye ni kiungo.
Ainembabazi tumemsajili kutoka Ceassia Queens ya Iringa ambaye anaijua vizuri Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier (SLWPL).
Mshambuliaji huyo anakuwa mchezaji watatu kusajiliwa kwenye kikosi cha Queens baada ya Diakiese isabelle na Nabbosa.
Tunaendelea kukisuka kikosi chetu kuelekea msimu mpya wa mashindano ambao unaanza mwezi ujao huku lengo letu likiwa kuchukua ubingwa wa SLWPL.