Queens yarejea mazoezini kujiandaa na Determine

Kikosi chetu leo jioni kimefanya mazoezi katika Uwanja wa Academia Fus Rabat kujiandaa na mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Determine Girls kutoka Libya.

Baada ya mchezo wa jana dhidi ya wenyeji ASFAR FC leo wachezaji wameendelea na program ya mazoezi kuweka miili sawa kujiandaa na mchezo huo ambao utapigwa Jumatano saa moja jioni kwa saa za nyumbani.

Wachezaji wote 25 wamefanya mazoezi ya leo na kizuri zaidi hakuna aliyepata majeraha kwenye mchezo wa jana ambayo yatamfanya kukosa mchezo wa Jumatano.

Ingawa tumeshindwa kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa jana morali ya wachezaji ipo juu na wapo tayari kuhakikisha tunapata ushindi ili kufufua matumaini ya kufuzu nusu fainali.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER