Queens yarejea kileleni mwa SLWPL kwa kishindo

Ushindi mnono wa mabao 4-1 uliopata Simba Queens dhidi ya Baobab Queens umetufanya kukamata usukani wa Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL).

Ushindi huo umetufanya kufikisha pointi 19 alama moja juu ya anayeshika nafasi ya pili huku timu zote zikiwa zimecheza mechi nane.

Hii ni mara ya kwanza msimu huu kuongoza kwenye msimamo kutokana na kutoanza vizuri katika mechi za mwanzo wa ligi.

Katika mchezo wa leo kiungo Vivian Corazone alitupatia bao la kwanza dakika ya 17 kabla ya Baobab kusawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 30 kupitia kwa Zainabu Rashid.

Nahodha Opa Clement alitupatia bao la pili dakika ya 32 na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuendelea kuliandama lango la Baobab huku wao wakifanya machache ya kushtukiza lakini umakini wa kutumia nafasi ulikuwa mdogo.

Jentrix Shikangwa alitupatia bao la tatu dakika ya 70 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Pambani Kuzoya.

Dakika ya 83 Corazone alitupatia bao la nne baada ya kuunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Asha Djafar.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Jentrix, Mwanahamisi Omary, Pambani na Corazone na kuwaingiza Aisha Juma, Asha Djafar, Joelle Bukuru na Asha Rashid.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER