Queens yapata mapokezi mazuri Morocco

Shirikisho la Soka nchini Morocco (FRMF) limetupatia mapokezi mazuri tangu tuwasili nchini hapa jana kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Hayo yamethibitishwa na Meneja wa Timu, Seleman Makanya na kuongeza kuwa mapokezi hayo ni kuanzia timu ilipowasili hapa Morocco ambapo walitupeleka hotelini tulipofikia huku taratibu zote stahiki zikifuatwa.

Makanya ameongeza kuwa pia Watanzania wanaoishi jijini Casablanca nao wametupatia mapokezi mazuri kiasi kwamba tunajiona tuko nyumbani Tanzania.

“Tumesafiri na wachezaji 25, tumefika salama Morocco jana jioni tunamshukuru Mungu tumepata mapokezi mazuri, hakuna changamoto yoyote tuliyokutana nayo mpaka sasa. FRMF imetupokea vizuri,” amesema Makanya.

Baada ya kuwasili jana wachezaji walipewa mapumziko na leo usiku wataanza rasmi mazoezi kujiandaa na michuano huku wakiendelea kuzoea mazingira.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER