Queens yapangwa na Yanga Princess Ngao ya Jamii

Ratiba ya Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii kwa timu za Wanawake imetoka na tumepangwa kucheza na Yanga Princess.

Michezo ya Ngao ya Jamii ni kiashiria cha kufunguliwa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Wanawake 2024/25.

Mchezo huo ambao utakuwa Nusu Fainali ya pili itapigwa Jumanne Septemba, 24 saa 10 jioni katika Uwanja wa KMC Complex.

Mshindi wa mchezo huo atacheza fainali na mshindi kati ya JKT Queens na Ceasia Queens ambao utapigwa Septemba 27 katika Uwanja wa KMC Complex.

Kikosi kinaendelea na mazoezi chini ya Kocha Mussa Hassan Mgosi kikiwa na lengo la kutwaa ubingwa wa taji hili ambalo sisi ndio Mabingwa Watetezi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER