Kikosi chetu cha timu ya Wanawake Simba Queens kimepangwa kundi B kwenye mechi za kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Queens imepangwa pamoja na timu za GRFC (DR Congo), SHE Corporate WFC (Uganda), YEI Joint Stars (Sudan ya Kusini).
Michuano hii ambayo inategemewa kuwa na upinzani mkubwa kutoka na ubora wa timu zote inatarajia kuanza Agosti 13-28 jijini Dar es Salaam.
Kundi A litakuwa na timu za CBE (Ethiopia), Warrior Queens (Zanzibar), FOFILA PF (Burundi), AS Kigali (Rwanda)