Queens yang’ara tuzo za TFF

Timu yetu ya Simba Queens imefanikiwa kunyakua tuzo tano katika hafla ya ugawaji iliyofanyika Hoteli ya Rotana jijini Dar es Salaam.

Queens imepata tuzo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake ‘Serengeti Lite Women’s Premier League’ (SLWPL).

Sebastian Nkoma amepata tuzo ya kocha bora wa mashindano baada ya kutuwezesha kutetea ubingwa wetu.

Mshambuliaji, kinara Asha Djafar ameshinda tuzo ya mfungaji bora wakati Fatuma Issa ‘Fetty Densa’ akichukua tuzo ya mchezaji bora wa msimu (MVP).

Mlinda mlango, Gelwa Yona amechaguliwa kipa bora wa mashindano kutokana na ubora mkubwa alio uonyesha.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER