Queens yang’ara Morocco

Kikosi chetu cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Determine Girls kutoka Liberia katika mchezo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mchezo ulianza kwa kasi huku tukishambuliana kwa zamu lakini safu zote za ushambuliaji zilishindwa kutumia nafasi ilizotengeneza.

Kipindi cha pili Kocha Charles Lukula aliwatoa Asha Mnuka na Vivian Corazone na kuwaingia Amina Ahmed na Olaiya Barakat ambao waliongeza kasi kwenye safu ya ushambuliaji.

Opa Clement alitupatia bao la kwanza dakika ya 53 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Olaiya muda mfupi baada ya kuingia.

Kocha Lukula aliwaingiza pia Dotto Evarist na Philomena Abakah kuchukua nafasi za Silvia Mwacha na Asha Djafar ambao nao waliifanya timu kuwa imara zaidi.

Olaiya alitupatia bao la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 79 baada ya Joelle Bukuru kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Nahodha wa Determine Margaret Stewart alitolewa kwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa ya pili ya njano baada ya kumchezea rafu Opa dakika ya 88.

Mchezo wetu wa mwisho wa hatua ya makundi utakuwa Jumamosi Novemba 5 dhidi ya Green Buffaloes kutoka Zambia.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER