Queens yakabidhiwa ubingwa kwa shangwe la Ushindi

Timu yetu ya Simba Queens imekabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Womens Premier League) kwa ushindi baada ya kuwafunga Baobab Queens mabao 3-0 mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Ubingwa huu tuliokabidhiwa ni watatu mfululizo huku tukiweka rekodi na kuonyesha tulikuwa bora kwa muda wote huo.

Pambani Kuzoya alitupatia bao la mapema dakika ya pili baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Baobab ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi ya kuliandama lango la Baobad ambapo nyota, Asha Djafar aliongeza bao pili dakika ya 50.

Joelle Bukuru alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la tatu dakika ya 90 na kuwafanya Baobab kuondoka uwanjani vichwa chini.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Olaiya Barakat, Vaileth Machela na Pambani na kuwaingiza Amina Ramadhani, Maimuna Khamis na Mercy Tagoe.

Queens imemaliza msimu ikiwa bingwa kwakufikisha pointi 63 baada ya kucheza mechi 22.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER