Queens yaishushia kipigo kizito Baobab

Kikosi chetu cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Baobab Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Joanitah Ainembabazi alitupatia bao la kwanza dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Dotto Everist.

Bao hilo halikudumu maana dakika ya 15 Elizabeth Edward baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango letu.

Asha Djafar alitupatia bao la pili dakika ya 31 baada ya kuuwahi mpira ambao wengi walidhani unatoka na kufunga.

Vivian Corazone alitupatia bao la tatu kutoka katika ya uwanja akipiga shuti kali liliomshinda mlinda mlango wa Baobab Jeanne Pauline.

Baobab walipata bao la pili dakika ya 51 kupitia kwa Daniela Ngoyi aliyejifunga kufuatia kurudisha mpira uliomshinda mlinda mlango, Carolyne Rufa.

Asha Djafar alitupatia bao nne dakika ya 64 kabla ya Asha Rashid ‘Mwalala’ kukamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la tano dakika ya 71.

Queens ilifanya mabadiliko ya kuwatoa Mwanahamisi Omary, Joanitah, Dotto, Djafar na Joelle Bukuru na kuwaingiza Diana Mnally, Elizabeth Wambui, Asha Rashid, Koku Kipanga na Jackline Albert.

SHARE :
Facebook
Twitter

One Response

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER