Queens yaipiga kitu kizito Oysterbay Queens

Timu yetu ya Wanawake Simba Queens, imeendelea kutoa dozi nzito kwa kila anayekutana naye baada ya kuichakaza bila huruma Oysterbay Queens mabao 7-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) uliofanyika Uwanja wa Uhuru.

Mabao sita yalipatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa wachezaji wawili Olaiya Barakat na Asha Djafar kila mmoja akipiga hat trick yake.

Olaiya alifunga mabao yake dakika za 5, 13 na 22 wakati Asha akifunga hat trick yake dakika za 10, 15 na 45.

Asha Djafar alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la saba dakika ya 75 na kuzamisha kabisa jahazi la Oysterbay.

Kocha Sebastian Nkoma alifanya mabadiliko ya kuwatoa mlinda mlango Gelwa Yohana nafasi yake ikachukuliwa na Janeth Shija huku Asha akitolewa na Mecy Tague akiingia.

Ushindi huu unatufanya kuendelea kusalia kwenye msimamo tukiwa na alama 39 baada ya kushinda mechi zote 13 za ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER