Queens yaipiga 4G Fountain Dodoma

Timu yetu ya Simba Queens imeendeleza moto wake katika Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Womens Premier League) baada ya kuichakaza Fountain Gate mabao 4-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

Tulianza mchezo kwa kasi ambapo ilituchukua dakika mbili kupata bao la kwanza lililofungwa na mshambuliaji kinara Asha Djafar baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Fountain.

Aisha Juma aliongeza bao la pili dakika ya 25 lililotufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 2-0.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kuendelea kuliandama lango la Fountain ambapo dakika ya 85 Asha Juma alitupia bao la tatu.

Wakati wengi wakidhani mchezo utamalizika kwa matokeo hayo, Jackline Albert alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne dakika ya 90.

Kocha Sebastian Nkoma alifanya mabadiliko ya kuwatoa Pambani Kuzoya na Asha Djafar na kuwaingiza Amina Ramadhani na Olaiya Barakat.

Matokeo haya yanatufanya kufikisha alama 51 baada ya kucheza mechi 18 tukiwa kileleni mwa msimamo alama saba juu ya anayetufuata huku tukisalia na mechi nne kabla ya kumaliza ligi.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER