Queens yaingia kambini kujiandaa na Ligi ya Mabingwa

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens itaingia kambini rasmi leo tayari kwa maandalizi ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika itayofanyika nchini Morocco kuanzia Oktoba 31 hadi Novemba 13.

Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Sebastian Nkoma kimeanza maandalizi mapema ili kuhakikishia tunakwenda kufanya vizuri kwenye michuano hiyo mikubwa barani Afrika.

Katika maandalizi hayo, leo saa 10 jioni kikosi kitafanya mazoezi katika Uwanja wa Mo Arena na baada ya hapo kitaingia kambini moja kwa moja.

Queens ambayo inawakilisha Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) imepangwa Kundi A pamoja na timu za Afsa FC (Morocco), Green Buffalo (Zambia) na Determine Girls (Libya).

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER