Queens yaifuata The Tigers Arusha

Kikosi chetu cha Simba Queens kimeondoka leo alfajiri kuelekea jijini Arusha tayari kwa mchezo wa pili wa Ligi ya Wanawake (Serengeti Lite Women’s Premier League) dhidi ya The Tigers Queens utakaopigwa Jumatano Uwanja wa Black Rhino, Karatu.

Queens imeondoka na kikosi cha wachezaji 27 ambapo baada ya kuwasili watapumzika na kesho watafanya mazoezi ya mwisho kabla ya kushuka dimbani Jumatano.

Meneja wa Timu, Seleman Makanya amesema mchezaji pekee aliyebaki Dar es Salaam ni Olaiya Barakat kutokana na maumivu aliyopata kwenye mchezo uliopita.

Makanya amesema baada ya kupoteza kwenye mchezo wa kwanza sasa mipango ni kuhakikisha tunashinda kila mechi tukianza Jumatano na The Tigers.

“Tumeanza safari alfajiri kuelekea Arusha kwa ajili ya mchezo wetu wa pili wa Ligi dhidi ya The Tigers utakaopigwa Jumatano, tumesafiri na kikosi kamili cha wachezaji 27 Olaiya pekee yake akibaki kutokana na majeraha,” amesema Makanya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER