Queens yaifuata Fountain Gate Dodoma

Kikosi chetu cha Simba Queens kimeondoka kuelekea jijini Dodoma tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Womens Premier League) dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Jumamosi Mei 7, mwaka huu.

Meneja wa timu Seleman Makanya amesema wamesafiri na kikosi kizima wakiwemo wachezaji waliokuwa kwenye majukumu ya Timu ya Taifa.

Makanya amesema hakuna mchezaji yeyote ambaye ni majeruhi au anayetumikia adhabu ya kadi hivyo benchi la ufundi litakuwa na wigo mpana wa kupanga kikosi.

Makanya ameongeza kuwa lengo letu ni kushinda kila mchezo ulio mbele yetu ili kujihakikishia nafasi ya kutetea ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

“Tumeanza safari ya kuelekea Dodoma kwa ajili ya mchezo wetu wa Ligi dhidi ya Fountain Gate utakaopigwa Jumamosi.

“Tumesafiri na kikosi kizima na benchi la ufundi hata wale wachezaji waliokuwa katika timu ya taifa, kikubwa tunawaomba mashabiki wetu wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti,” amesema Makanya.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER