Simba Queens imeondoka asubuhi kuelekea mkoani Iringa kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) dhidi ya Ceasiaa Queens.
Mchezo dhidi ya Ceasiaa Queens utapigwa Jumatano saa 10 jioni katika Uwanja wa Chuo Kikuu cha Mkwawa ambao ni muhimu kwetu kupata ushindi ili kufufua matumaini ya ubingwa.
Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri tayari kupambana hadi tone la mwisho kuhakikisha tunashinda ingawa tunaamini utakuwa mgumu.
Queens itaingia kwenye mchezo wa Jumatano ikiwa nafasi ya pili katika msimamo na pointi 42 alama moja nyuma ya vinara JKT Queens.