Queens yaichapa Yanga Princess Tamasha la Wanawake

Timu yetu ya Wanawake ya Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Yanga Princess katika mchezo wa kuhitimisha Tamasha la Kimataifa la Wanawake lililofanyika Uwanja wa Uhuru.

Mchezo ulianza kwa kasi ya kawaida tukishambuliana kwa zamu huku mpira ukichezwa zaidi eneo la katikati ya uwanja.

Safu yetu ya kiungo ya ushambuliaji iliyokuwa chini ya Joelle Bukuru, Olaiya Barakat na Asha Djafar ilijitahidi kutengeneza nafasi ingawa Princess walikuwa makini.

Opa Clement alitufungia bao la kwanza kwa kichwa baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na kiungo Vivian Corazone dakika 67.

Mshambuliaji Jentrix Shikangwa aliyeingia kutokea benchi alitupatia bao la pili dakika ya 88 baada ya kumalizia pasi ya Asha Djafar.

Kocha wa Queens Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Olaiya Barakati na Pambani Kuzoya na kuwaingiza Jentrix Shikangwa na Topista Situma.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER