Queens yaichapa Mkwawa 4G Uhuru Dar

Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Mkwawa Queens kutoka Iringa katika mchezo wa Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League (SLWPL) uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mchezo huo ulianza kwa kasi ya kadiri huku tukifika zaidi langoni mwa Mkwawa lakini waliweza kutuhimili katika dakika 15 za kwanza.

Shikangwa tena alitupatia bao la pili dakika ya 30 kwa shuti kali la mguu wa kushoto baada ya kupokea pasi kutoka kwa Asha Mwalalala.

Jentrix Shikangwa alitupatia bao kwanza dakika Ya 19 baada ya beki wa Mkwawa, Winfirda Nicholaus kupiga kichwa cha Nyuma kumrudishia golikipa wake kabla ya mpira kumkuta mfungaji.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kuendelea kulisakama lango la Mkwawa lakini mashambulizi hayakufanya kubadili ubao wa matokeo kwenye dakika 30 za mwanzo.

Vivian Corazone alitupatia bao la tatu dakika ya 80 akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Wema Richard.

Zainabu Mohamed alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la nne dakika ya 88 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Jentrix.

Kocha mkuu Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Fatuma Issa, Diana Mnaly, Vivian na Asha Mlangwa na kuwaingiza Koku Kipanga, Zainabu Mohamed, Joelle Bukuru na Olaiya Barakat.

Ushindi wa leo unatufanya kufikisha pointi 33 tukirejea kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 14.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER