Queens yaichapa Fountain Uhuru

Kikosi chetu cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite Women’s Premier League uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Fountain walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 15 kupitia kwa Ritticia Nabbosa kwa kichwa baada ya walinzi wetu kuzembea kuokoa mpira wa kona.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya mapema dakika ya 20 ya kumtoa mlinzi wa kati Daniela Mgoyi na kumuingiza Esther Mayala.

Nahodha Opa Clement alitusawazishia bao hilo kwa mkwaju wa penati dakika ya 31 baada ya Jentrix Shikangwa kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Asha Djafar alitupatia bao la pili dakika ya 61 shuti kali ndani ya 18 baada ya kutengwa na Opa mpira wa krosi uliopigwa na Shikangwa.

Kipindi cha pili Kocha Lukula aliwatoa Diana Mnali na Pambani Kuzoya na kuwaingiza Aisha Juma na Amina Ramadhani.

Ushindi wa leo unatufanya kufikisha pointi saba baada ya kucheza mechi nne tukishinda mbili, sare moja na kupoteza moja.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER