Queens yaichapa Fountain Jamhuri Dodoma

Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi ya Wanawake Serengeti Lite Women’s Premier League kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mchezo huo ilikuwa mkali huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini wenyeji Fountain walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 16 lililofungwa na Neema Paul kufuatia mlinda mlango wetu Caroline Rufa kufanya makosa.

Baada ya bao hilo mchezo ulizidi kuwa mkali huku mashambulizi yakiendelea pande zote lakini matokeo hayakubadilika mpaka tunaenda mapumziko.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo Jentrix Shikangwa alitupatia bao la kusawazisha kwa mkwaju wa penati dakika ya 70 kufuatia Asha Djafar kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Dakika tano baadae Shikangwa alikosa mkwaju wa penati kufuatia yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Mlinzi wa kati Ruth Ingosi alitupatia bao la ushindi dakika ya 84 kwa shuti kali nje ya 18 kufuatia mpira kuzuiwa na walinzi wa Fountain kabla ya kumkuta.

Kocha Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Pambani Kuzoya, Zainabu Mohamed na Joelle Bukuru kuwaingiza Diana Mnali, Asha Djafar na Mwanahamisi Omary.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER