Queens yaichapa Amani Queens Uhuru

Simba Queens imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Amani Queens katika mchezo wa Serengeti Lite Women’s Premier League uliopigwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo ulianza kwa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu ingawa tulimiliki sehemu kubwa.

Mkongwe Asha Mlangwa ‘Mwalala’ alitupatia bao la kwanza dakika ya 37 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Wema Richard.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo dakika ya 60 Asha Djafar alipachika bao la pili kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda mlango wa Amani.

Kocha Mkuu, Charles Lukula alifanya mabadiliko ya kuwatoa Mwalala, Vivian Corazone, Diana Mnali na Danai Bhobho na kuwaingiza Zainabu Mohamed, Pambani Kuzoya, Topister Situma na Mwanahamisi Omary.

Ushindi huu umetufanya kufikisha pointi 36 baada ya kucheza mechi 15 tukiwa nafasi ya pili.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER