Queens yaichakaza TSC, Djafar atupia manne

Timu yetu ya Simba Queens imeendeleza umwamba katika Ligi Kuu ya Wanawake (Serengeti Lite Womens Premier League) baada ya kuichapa bila huruma TSC Queens mabao 6-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Mo Simba Arena.

Tulianza mchezo kwa kasi ambapo Amina Ramdhani alitupatia bao la kwanza dakika ya nane baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa TSC.

Asha Djafar alitupia bao la pili dakika ya 15 kabla ya kuongeza la tatu dakika ya 30 na kutufanya kwenda mapumziko tukiwa mbele kwa mabao 3-0.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi ambapo ilituchukua dakika 10 kabla ya Pambani Kuzoya kutupatia bao la nne.

Djafar alitupatia bao la tano dakika ya 75 likiwa ni la tatu kwake katika mchezo (hat trick) kutokana na uwezo mkubwa alioonyesha mbele ya walinzi wa TSC.

Wakati mpira unaelekea ukingoni Djafar alikamilisha karamu ya mabao kwa kutupia la sita dakika ya 90 likiwa ni la nne kwake katika mchezo.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Mercy Tagoe, Maimuna Khamis na Violeth Thadeo na kuwaingiza Olaiya Barakat, Silvia Mwacha na Zubeda Mgunda.

Ushindi wa leo umetufanya kufikisha alama 48 tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 17 tukishinda 16 na kupoteza mmoja pekee.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER