Queens yaichakaza The Tigers Arusha

Timu yetu ya Simba Queens imeendeleza moto wake katika Ligi ya Wanawake Serengeti Lite Womens Premier League baada ya kuichapa The Tigers Queens mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Mchezo ulianza kwa kasi tulishambulia lango lango la The Tigers ambapo dakika ya 20 Asha Djafar alitupatia bao la kwanza ambalo lilidumu mpaka mapumziko.

Kipindi cha pili tuliongeza kasi na kufanya mashambulizi ambapo dakika ya 60 Falone Pambani alitupatia bao la pili akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na Asha Djafar.

Kiungo Joelle Bukuru alikamilisha karamu ya mabao kwa kufunga la tatu dakika ya 70 kwa mkwaju wa penati baada ya yeye mwenyewe kufanyiwa madhambi ndani ya 18.

Kocha Sebastian Nkoma aliwatoa Amina Ramadhani na Asha Djafar na kuwaingiza Olaiya Barakat pamoja na Mercy Tagoe.

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 54 tukiwa kileleni mwa msimamo baada ya kucheza mechi 19.

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER