Queens yaichakaza Alliance bila huruma

Kikosi cha Simba Queens kimefanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Alliance Girls katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake uliopigwa katika Uwanja wa Azam Complex.

Mchezo huo ulitawaliwa na mbinu nyingi huku kila timu ikifanya mashambulizi ya mipango na kujilinda kwa pamoja hali iliyopelekea kwenda mapumziko bila kufungana.

Kipindi cha pili kocha msaidizi Mussa Mgosi alibadili mbinu na kuanza kucheza soka la kasi na kuwafanya Alliance kufanya makosa mengi ambayo tuliyatumia na kupata ushindi mnono.

Mabao yetu yalifungwa na Jentrix Shikangwa aliyefunga matatu ‘hat trick’ Asha Djafar aliyefunga mawili huku Aisha Juma na Vivian Corazone wakifunga moja kila mmoja.

Ushindi huu leo ndio mkubwa zaidi tangu tuliopoanza ligi msimu huu ambao umetufanya kufikisha pointi 16 baada ya kucheza mechi sita.

Kocha Mgosi alifanya mabadiliko ya kuwatoa Dotto Evarist, Carolyene Rufa, Fatuma Issa, Ritticia Nabbosa na Elizabeth Wambui na kuwaingiza Gelwa Yona, Olaiya Barakat, Mwanahamisi Omary, Danai Bhobo na Esther Mayala

SHARE :
Facebook
Twitter

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

GET NEWSLETTER